Tiketi Mtandao ni programu ya kilelektroniki kwa ajili ya ukataji wa tiketi za mabasi nchini Tanzania kimtandao. Programu hii itamruhusu mtu yeyote nchini Tanzania kuweza kukata tiketi bila uhitaji wa kwenda kwenye ofisi za kampuni ya basi, malipo baadaye yatalipwa kwa kutumia mitandao ya simu au huduma za kibenki.
Una mpango wa kusafiri katika siku za usoni? NIDC kwa kushirikiana na LATRA na TRA, imezindua rasmi Tiketi Mtandao. Suluhisho ya malipo kimtandao inayokuwezesha kuweka nafasi na kulipia tiketi za basi za masafa marefu kupitia simu yako kiganjani. Ni rahisi sana, BONYEZA, LIPA, SAFARI!